SIMBA WAIREJESHA TUZO KWA MASHABIKI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa tuzo ya mashabiki bora ambayo wamepata kutokana na kushiriki michuano ya African Football League ni heshima kubwa kwao.

Ikumbukwe kwamba Simba iligotea hatua ya robo fainali kwa kuondolewa na Al Ahly ya Misri. Baada ya kutwaa tuzo hiyo walibainisha kuwa ni ya kila shabiki wa Simba.

Novemba 11 Simba walikabidhiwa tuzo hiyo Afrika Kusini katika fainali ya pili iliyochezwa Uwanja wa Loftus Versfeld ambapo mabingwa wa michuano hiyo mipya waliibuka kuwa ni Mamelod mbele ya Wydad Casablanca.

Ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Muhene, (Try Again) alikabidhiwa tuzo hiyo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa jambo hilo ni kubwa na linaleta heshima

Try again amesema: “Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu.,”