SIMBA YAGAWANA POINTI NA NAMUNGO NYUMBANI

KIKOSI cha Simba kimegawana pointi moja na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Simba 1-1 Namungo ikiwa ni mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Namungo walianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa Relliats Lusajo.

Lusajo alifunga bao hilo dakika ya 29 ya mchezo kutokana na makosa ya wachezaji wa Simba kwenye kuokoa hatari.

Kwa upande wa Simba ni Jean Baleke amefunga bao hilo dakika ya 75.