KIVUMBI CHA LIGI KUU BARA KIPO HIVI

KIVUMBI cha Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 kinaendelea ikiwa ni wiki ya 8 kwa timu kushuka uwanjani kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Singida Fountain Gate leo watakuwa nyumbani baada ya kutoka kucheza mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Watamenyana na Ihefu kwenye mchezo wa leo Novemba Mosi Uwanja wa Liti.

Mashujaa kutoka Kigoma timu yenye ukuta mgumu kupitika kwa sasa msimu wa 2023/24 ikiwa imetunguliwa mabao matatu pekee watamenyana na Azam FC yenye Feisal Salum Uwanja wa Lake Tanganyika.

Coastal Union ya Tanga itamenyana na Namungo Uwanja wa Mkwakwani.

Happy new month Novemba