MCHEZO wa El Clasico, Barcelona wameshuhudia wakipoteza pointi tatu mazima ndani ya Uwanja wa Camp Nou.
Ulikuwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, (La Liga) uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Barcelona 1-2 Real Madrid ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa miamba hawa wa Hispania kukutana msimu wa 2023/24
Ni Ikay Gundogan alianza kupachika bao dakika ya tano kwa Barcelona, mwamba Jude Bellingham alisawazisha dakika ya 68 na dakika ya 90+2 akamalizia bao la pili la pointi tatu kwa Real Madrid.