NYOTA WA YANGA AIOMBEA DUA SIMBA DHIDI YA WAARABU

FISTON Mayele nyota wa zamani wa Yanga amesema kuwa anawaombe kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye African Football League Simba wapate matokeo mazuri.

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Roberto Oliveira leo Oktoba 24 kina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Al Ahly.

Makosa ya safu ya ulinzi kwa Simba yaliigharimu timu hiyo kulinda ushindi wa bao la pili lililofungwa na Sadio Kanoute kwa pigo la kichwa akitumia pigo la kona iliyopigwa na Saido Ntibanzokiza.

Mayele kwa sasa yupo nchini Misri akikipiga ndani ya Klabu ya Pyramids ya Misri ana marafiki ndani ya Simba kwa kuwa alipokuwa Yanga walikuwa ni watani zao wa jadi.

Mayele amesema: “Nipo Misri na nipo kwa marafiki zangu Simba ambao wanamchezo dhidi ya Al Ahly ninawaombea matokeo mazuri kwenye mchezo wao,”.