Kipindi cha pili ubao umesoma Al Ahly 1-1 Simba ambapo Simba walipachika bao kupitia kwa Sadio Kanoute dakika ya 67 likasawazishwa na Kahraba dakika ya 76.
FT Al aHLY 1-1 Simba na wanaondolewa kwa kanuni kwa kuwa mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani waliruhusu kufungwa mabao 2-2.
Ni hatua ya robo fainali, African Football League nchini Misri dakika 45 ubao ulisoma Al Ahly 0-0 Simba kipindi cha kwanza.
Ndani ya dakika 45 Al Ahly wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kumfuata Ally Salim ambaye yupo langoni.
Kwa upande wa Simba wao wanamtumia Kibu Dennis na John Bocco kwenye upande wa ushambuliaji na viungo ni Clatous Chama, Saido Ntibanzokiza kwenye kutengeneza mipango.
Beki Mohamed Hussein anaingia kwenye orodha ya nyota waliopiga shuti lililolenga lango kwenye mchezo wa leo.
Jumla ni mabao 2-2 ambayo wamefungana wababe hawa nafasi kubwa ya kusonga mbele ikiwa mataokeo yatakuwa hivi ni kwa wenyeji Al Ahly waliopata mabao ya ugenini.