Home Sports PIRA PAPATUPATU LAKOMBA POINTI UGENINI

PIRA PAPATUPATU LAKOMBA POINTI UGENINI

KUTOKANA na mashabiki wa Simba kueleza kuwa mpira unaochezwa kwa sasa chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ni mwendo wa papatupapatu, hivyo zimejibu na kupata ushindi ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti umesoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba.

Bao la Saido Ntibanzokoza dakika ya 26 lilikuwa la mipango na bao la pili la Moses Phiri ambaye pigo hilo lilimshinda Beno Kakolanya.

Bao la Singida Fountain Gate lilifungwa na Deus Kaseke kutokana na makosa ya Ally Salim kàtika kuokoa hatari

Pointi 15 ikiwa inaongoza ligi wanafikisha Simba baada ya kucheza mechi tano msimu wa 2023/24.

Bado ligi ni mbichi na bingwa mtetezi Yanga naye ana kasi ya kupata matokeo kwa kuwa mchezo uliopita ni mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold ilishinda ugenini.

Previous articleMKWANJA WA MAMA MIKONONI MWA TIMU YA TAIFA
Next articleKAZI KIMATAIFA NI KUBWA MIPANGO MUHIMU