MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amekiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25.
Atakuwa shuhuda wa kujua kundi atakalokuwa leo Oktoba 6 jijini Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa ni tukio la kupangwa kwa droo ya hatua ya makundi kimataifa kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa Simba ni Kocha Mkuu, Roberto Oliveira atakuwa shuhuda wa kuwatambua wapinzani wake kwenye anga la kimataifa.Timu mbili kutoka ardhi ya Tanzania zipo hatua hiyo ikiwa ni Yanga na Simba.
Poti zipo nne kuendana na wingi wa poiñti ambazo timu hizo 16 zumekusanya katikà michuano ya kimataifa.
Poti 1
Al Ahly, Mamelodi, Esperance, Wydad Casablanca.
Poti 2
Simba, CR Belouzdad, Petro Atletico, Pyramid
Poti 3
Yanga, TP Mazembe, ASEC Mimosas, Al Hilal
Poti 4
Jwaneng Gallaxy, Medeama, Etoile Du Sahel, FC Nouadhibou.