REKODI MPYA KWA YANGA KIMATAIFA

HATIMAYE Yanga imetinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupita miaka 25.

Ushindi wa bao 1-0 Al Merrikh, Uwanja wa Azam Complex umewapa tiketi ya kuvunja rekodi hiyo.

Bao la mzawa Clement Mzize dakika ya 66 limetosha kuwapa ushindi Yanga kwenye mchezo wa nyumbani.

Ni ushindi wa jumla ya mabao 3-0 Yanga inapenya kwa kuwa mchezo wa kwanza ugenini ilipata ushindi wa mabao 2-0.

Kwenye mchezo wa ugenini mabao ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda ambaye ni raia wa Zambia na bao jingine ni mali ya Mzize.

Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili mfululizo dhidi ya Al Merrikh bila ukuta wao kuruhusu nyavu kutikisika.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa kazi kubwa kwa wachezaji ni kutafuta ushindi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

“Kikubwa ni kupata ushindi na wachezaji wanajituma hili ni jambo kubwa tuna amini tutaendelea kuwa kwenye mwendo mzuri,”.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao walianza kikosi cha kwanza ni pamoja na Aziz KI, Mudhathir Yahya, Joyce Lomalisa.