PHIRI: TUNAFUNZU HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mzambia, Moses Phiri ametamba kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajii ya mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos, huku akitamba kuwa Simba itaibuka na ushindi na kufuzu makundi ya mashindano hayo.

Simba leo Jumapili watakuwa wenyeji wa Dynamos katika mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

Ni mashuhuda wa watani zao wa jadi Yanga wakikamilisha rekodi ya kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 Al Merrikh.

Simba wataingia katika mchezo huo wakiwa na uhitaji wa angalau sare ya bao 1-1 ili kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo, hii ni kufuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2 waliyoipata kwenye mchezo wa ugenini.

 Phiri amesema: “Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huu, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hasa kutokana na ubora wa wapinzani wetu na matokeo ya mchezo wa awali kule Zambia.

“Hivyo kila mchezaji anajua nini wajibu wake na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kwenda hatua ya makundi akili zetu zipo kwenye kuhakikisha tunafanikisha hilo, tupo tayari.”