Home Uncategorized MWAMBA AJAZWA UPEPO SIMBA ATUMA UJUMBE KWA WAZAMBIA

MWAMBA AJAZWA UPEPO SIMBA ATUMA UJUMBE KWA WAZAMBIA

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewaambia washambuliaji wake wakiongozwa na Jean Baleke kutumia vyema kila nafasi watakayoipata ili wapate bao la mapema ndani ya dakika 10 kuwavuruga wapinzani wao Power Dynamos ya nchini Zambia.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana leo Jumapili saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar.

Mchezo huo ni ule wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ule wa kwanza Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

 Robertinho amesema kuwa hataki kuona makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita yakijirudia tena watakaporudiana dhidi ya Power Dynamos.

Robertinho amesema kuwa umakini mdogo wa washambuliaji akiwemo Baleke, ndio ulisababisha wakose ushindi katika mchezo uliopita, hivyo amewaongezea mbinu na kuwapa maelekezo washambuliaji wake umuhimu wa kutumia nafasi za kufunga.

Aliongeza kuwa anaamini timu yake itapata ushindi katika mchezo huo na kufuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, hilo linawezekana kutokana na kurekebisha makosa waliyoyafanya katika mchezo uliopita.

“Nimefanya maboresho ya kikosi changu katika kila sehemu, lakini kubwa ya ushambuliaji ambayo ndio ilisababisha tukose ushindi ugenini tulipocheza dhidi ya Power Dynamos.

“Nimewapa mbinu na maelekezo wachezaji wangu zitakazowafanya kufunga mabao mengi katika mchezo, kikubwa nimesisitiza kutumia kila nafasi tutakayoipata kufunga mabao.

“Kama unavyofahamu katika michuano hii, nafasi ni chache zinazopatikana, hivyo ni lazima kuzitumia vema kwa kufunga, ninaamini hatutapata nafasi nyingi katika mchezo huu wa marudiano, kwani wapinzani watacheza kwa tahadhari ya kujilinda wapo ugenini,” amesema Robertihno.

Previous articleYANGA YAVUNJA REKODI YAKE KIMATAIFA
Next articleREKODI MPYA KWA YANGA KIMATAIFA