Home Sports SIMBA KWENYE KAZI NZITO KIMATAIFA, MABAO YA KIDEO TATIZO

SIMBA KWENYE KAZI NZITO KIMATAIFA, MABAO YA KIDEO TATIZO

KAZI ni nzito kwa wachezaji wa Simba kusaka ushindi mbele ya Power Dynamos katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Oktoba Mosi.

Ikiwa wachezaji wataingia uwanjani kutafuta mabao ya kideo itawagharimu na safari ya kutinga hatua ya makundi itagotea hapo.

Hasara kubwa kwa Simba kutokana na uwekezaji katika usajili msimu wa 2023/24 hasara kwa Taifa kubaki na Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika Singida Fountain Gate wanakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Future huku Yanga wakiwa wameandika rekodi nzuri kimataifa.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa ugenini ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba. Ipo wazi kuwa wachezaji wa Simba walipata nafasi zaidi ya nne na kukwama kuzitumia. Miongoni mwao ni pamoja na mshambuliaji Jean aleke aliyeonekana kuhitaji kufunga mabao ya kiufundi, (mabao ya kideo).

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ameweka wazi kuwa walipata nafasi nyingi wakashindwa kuzitumia jambo ambalo wamelifanyia kazi.

“Katika mchezo uliopita tulipata nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia hivyo kwa mchezo wetu ujao tutakuwa makini na tunahitaji ushindi kutinga hatua ya makundi,”amesema Oliveira.

Previous articleFT: LIGI YA MABINGWA AFRIKA: SIKILIZA YANGA 1-0 AL MERRIKH
Next articleYANGA YAVUNJA REKODI YAKE KIMATAIFA