ROBERTINHO AKOLEZA DOZI SIMBA

ROBERTO Oliveira ‘Robertinho’ Kocha Mkuu wa Simba, ameweka wazi kuwa, kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni wachezaji wote kuongeza kasi na umakini wawapo ndani ya eneo la 18.

Timu hiyo ipo katika maandalizi ya mechi za kitaifa na kimataifa kwa msimu wa 2023/24, pia inapambana kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

Mazoezi ya Simba yanafanyika Simba Mo Arena ikiwa ni program zinazoandaliwa na benchi la ufundi la timu hiyo iliyo nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara.

Robertinho amesema: “Kila wakati tunafanyia kazi makosa yaliyopita ili kuwa imara na tunatambua kwamba katika kufikia malengo ni muhimu kufanya yote kwa umakini.

“Kuanzia safu ya ushambuliaji na ulinzi kote ni muhimu kufanya kazi kwa umakini katika kutafuata matokeo chanya uwanjani na inawezekana.”