Home Sports COASTAL UNION INAJITAFUTA KIMATAIFA

COASTAL UNION INAJITAFUTA KIMATAIFA

UONGOZI wa Coastal Union umesema  utahakikisha kuwa unafanya vizuri kwenye ligi kuu msimu huu ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mpaka  sasa kwenye ligi Coastal Union ipo nafasi ya 10 ina pointi moja baada ya kucheza michezo miwili baada ya kupoteza  mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja.

Timu hiyo iliwahi kucheza fainali ya Azam Sports Federation a kugotea washindi wa pili huku ubingwa ukiwa mikononi mwa Yanga.

Yanga ilishinda mchezo huo kwa penalti baada ya kufungana mabao 3-3 kwenye mchezo huo.

Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kuinoa Yanga na Polisi Tanzania kwa nyakati tofauti.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas El-Sabri alisema kuwa uongozi una malengo makubwa inayofanyia kazi kwa msimu mpya.

“Tuna malengo ya kufanya vizuri kwenye ligi ili kushiriki mashindano ya kimataifa na hilo linatufanya tufikirie kumaliza ndani ya nafasi nne za juu.

“Pia tunamalengo ya kuchukua taji la Azam Sports Federation hilo linawezekana kwa kuwa tuna nia ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao,”.

Previous articleMAXI, PACOME WAITEKA RWANDA,ROERTINHO ASHUSHA NONDO NZITO KWA LUIS
Next articleYANGA YAINGIA ANGA ZA WAARABU, BOSI ATANGAZA KUMWAGA PESA