KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi
amesema kuwa anafurahi kuona mshambuliaji
wake mpya, Hafiz Konkoni anaanza kufunga
mabao ndani ya timu hiyo huku akiamini
makubwa kutoka kwa mchezaji huyo.
Konkoni ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo
ametoka katika klabu ya Bechem United ya
Ghana ambapo tayari ameanza kufungua
akaunti ya mabao ndani ya Yanga baada ya
kufunga bao katika mchezo wa ligi dhidi ya
KMC.
Kocha wa Yanga amesema kitendo cha kufunga bao kwa Konkoni kimemfurahisha kwa kuwa kitampa hali nzuri ya kuendelea kujiamini kwa kumpunguzia presha ambayo pengine
angeendelea kuwa nayo ya kucheza bila kupata
bao jambo ambalo kwake anazidi kupata
matumaini makubwa.
“Kwa mchezaji ambaye anacheza katika eneo la ushambuliaji kitendo cha kucheza michezo
mitatu bila kufunga bao ni jambo ambalo
humpa mawazo mshambuliaji yeyote, kwa
watu wanaocheza nafasi za ushambuliaji furaha
yao kubwa ni kuweza kuhakikisha kuwa
wanafunga mabao mengine hayo ni baadae.
“Ndio maana hata kwa upande wangu
nimefurahi kumuona mshambuliaji wangu
akifunga bao kwa kuwa naamini itamuongezea
nguvu ya kupambana na kujiamini kwani
itamuondolea ile presha ambayo angeweza
kukutana nayo au kumkumba pale ambapo
angeshindwa kufunga katika michezo ijayo.
Mimi binafsi naamini kuna makubwa kutoka
kwake.”