UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo wa leo wa kimataifa dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia.
Ikumbukwe kwamba ni timu nne ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara zinaipeperusha bendera anga la kimataifa ikiwa ni Yanga na Simba hizi ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam FC inatarajia kutupa kete yake ya pili Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Katika mchezo wa kwanza ubao ulisoma Bahir Dar Kenema 2-1 Azam FC na bao la Azam FC lilijazwa kimiani na Idris Mbombo.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema, “Tukutane kwa wingi Azam Complex kwenye siku ya kisasi.
“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki na kuwapa kile ambacho wanastahili,”.
Miongoni mwa wachezaji wa Azam FC ambao wapo kwenye maandalizi ya mchezo huo ni pamoja na Feisal Salum aliyeibuka hapo akitokea kikosi cha Yanga sawa na Yannick Bangala.