Home Sports SIMBA WANA JAMBO LAO

SIMBA WANA JAMBO LAO

BAADA ya kucheza mechi mbili Simba imekusanya pointi sita ikiwa inaongoza ligi.

Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira katika mchezo wa kwanza ilitunguliwa mabao mawili dhidi ya Mtibwa Sugar licha ya kushinda.

Baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtiwa Sugar 2-4 Simba.

Katika mchezo wa pili ni ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Miongoni mwa nyota ambao wamekuwa wakipewa nafasi na kocha ni pamoja na mfungaji bora msimu wa 2022/23 Saido Ntibanzokiza.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa watapambana kufanya vizuri.

“Tunatamua ushindani ni mkubwa tupo tayari na tutafanya yote kwa umakini kufikia malengo,”.

Previous articleYANGA 1-0 KMC, LIGI KUU BARA
Next articleYANGA WAFANYA KWELI YAPIGA 5G