MCHEZO wa kwanza katika Kombe la Shirikisho Azam FC imeanza kwa kupoteza baada ya dakika 90 kukamilika.
Ikiwa ugenini imeshuhudia ubao ukisoma Bahir Dar 2-1 Azam FC hivyo wana kazi ya kusaka ushindi mchezo wa pili ili kuongeza nafasi ya kusonga hatua inayofuata katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Bao la Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabi limefungwa na Idris Mbombo dakika ya 72.
Bao hilo limeongeza angalau nguvu ya Azam FC kupambana kwa mchezo ujao baada ya kutaguliwa na mabao mawili yaliyofungwa na nyota mmoja wa wapinzani.
Ni Fitsum Gebre huyu alimtungua Idrissu Abdulai mabao yote ilikuwa dakika ya 20, 60.
Marudio itakuwa ni Agosti 25 Uwanja wa Azam Complex.