Home Sports MTIBWA SUGAR WATUMA UJUMBE HUU SIMBA

MTIBWA SUGAR WATUMA UJUMBE HUU SIMBA

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umebainisha kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi ya msimu mpya wakiwa tayari kwa mechi zote zinazowahusu.

Timu hiyo inatumia Uwanja wa Manungu kwa mechi za nyumbani. Mchezo wake wa kwanza ni dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Agosti 17.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na wanaimani ya kufanya vizuri.

“Tupo tayari kwa mechi zote ambazo tutacheza hatuhofii ndio maana tupo kwenye ligi sio Yanga, Simba au Azam FC tunatambua lazima tucheze na timu zote.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu nasi tunafanya maandalizi kupata matokeo mazuri. Makosa ambayo yalifanyika msimu wa 2022/23 hayo benchi la ufundi linafanyia kazi,” amesema Kifaru.

Ufunguzi wa msimu wa 2023/24 ulitanguliwa na mechi za Ngao ya Jamii ambapo timu nne zilishiriki Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Yanga, Simba, Azam FC na Singida Fountain Gate hizi zilishiriki mashindano haya yaliyokuwa na ushindani mkubwa.

Ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto oliveira ilitwaa taji hilo mbele ya watani zao wa jadi Yanga.

Mtibwa Sugar wakati wa maandalizi ya msimu mpya ilicheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na KMC, AS Vita ikiwa ni kwa ajili ya kuimarisha timu hiyo.

Previous articleMUDA WA KAZI NI SASA KWA KILA TIMU KUFANYA KWELI
Next articleMCHONGO WA YANGA CAF HUU HAPA, KIUNGO SIMBA ATIMKA