Home Sports IHEFU YAANZA KWA KUPOTEZA LIGI KUU BARA, GEITA KICHEKO

IHEFU YAANZA KWA KUPOTEZA LIGI KUU BARA, GEITA KICHEKO

GEITA Gold inaandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kukomba pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Ni Agosti 15 rasmi ligi  imeanza ambapo Geita Gold walikuwa ugenini walipokaribishwa na Ihefu.

Ikumukwe kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga ambao walitwaa taji hilo wakiwa na jumla ya pointi 78.

Yanga walikuwa tofauti ya pointi tano na watani wa jadi Simba waliogotea nafasi ya pili na pointi 73.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Higland Estate, Mbeya umesoma Ihefu 0-1 Geita Gold.

Bao pekee la ushindi limejazwa kimiani na Elias Maguli nyota wa Geita Gold dakika ya tano.

Kwenye mchezo huo wa leo ni dakika sita ziliongezwa kwa timu zote kuonyesha makeke yao na hakuna iliyopata bao kwenye kipindi hicho cha nyongeza.

Previous articleMAUA YA MKWAKWANI YAMWAGIWE KIRUMBA, ALI HASSAN MWINYI
Next articleYANGA YAIPIGIA HESABU ASAS DJIBOUT