ARSENAL WAMEANZA KWA KASI

WAMEANZA kwa kujiamini washika bunduki Arsenal mbele ya wapinzani wao Manchester City.

Ni katika mchezo wa Ngao ya Jamii walifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 4-1.

Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa walitoshana nguvu kwa kifungana bao 1-1.

Ilibaki kidogo wapishane na taji hilo kwani walisubiri hadi dakika ya 90+11 kusawazisha kupitia kwa Leandro Trossard aliyetokea benchi dakika ya 75.

Ni Cole Palmer alikuwa wa kwanza kufunga dakika ya 77 Uwanja wa Wembley na walipofika katika penalti Kevin de Bryune na Rodri walikosa huku Bruno Silva pekee alifunga.

Ni Martin Odegaard, Leandro Trossard, Bukayo Saka na Fabio Viera walifunga.