Home Sports SINGIDA FOUNTAIN GATE WAPANIA KUFANYA VIZURI

SINGIDA FOUNTAIN GATE WAPANIA KUFANYA VIZURI

TIMU ya Singida Fountain Gate inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara inaendelea na maadalizi kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu 2023/2024.

Singida Fountain Gate iliweka kambi Arusha ilirejea Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya tamasha la Singida Big Day.

Tamasha la Singida Big Day lilifanyika Agosti 2 2023 na walitambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2022/23.

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema: “Timu yetu inajiandaa vyema na msimu ujao tukiwa na mikakati mizuri.

“Hakuna majeruhi kwa sasa wachezaji wanaendelea vizuri na mazoezi tunaomba mashabiki watuunge mkono katika mashindano ninaimani tutafanya vizuri katika mashindano ya ligi.

“Mpago mkubwa ni kufanya vizuri kwenye mashindano ambayo tunashiriki. Wachezaji wapo tayari na tunaamini itakuwa hivyo licha ya ushindani kuwa mgumu tupo tayari,”.

Timu hiyo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ina kibarua cha kucheza Ngao ya Jamii ikianza hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Agosti 5 Singida Fountain Gate waliwasili Tanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya Ngao ya Jamii.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Beno Kakolanya, Meddie Kagere, Joash Onyango.

Previous articleAMANI ITAWALE KWENYE KILA ENEO SIMBA DAY
Next articleSIMBA YAANZA KWA USHINDI DHIDI YA POWER DYNAMO