Home Sports MASTAA HAWA WAMPA JEURI GAMONDI

MASTAA HAWA WAMPA JEURI GAMONDI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina anatajwa kuwa kwenye furaha kuwaona makipa watatu wakiwa kwenye uimara mazoezini.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwenye upande wa makipa wapo watatu ikiwa ni Djigui Diarra raia wa Mali huyu ni kipa namba moja.

Djigui ana tuzo ya kipa bora na yupo kwenye orodha ya kikosi bora msimu wa 2022/23 wengine ni Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery ambao hawa ni wazawa.

Taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa makipa wote wanampa furaha Gamondi kambini kutokana na kuwa makini kutimiza majukumu yao.

“Kocha anafurahia uwepo wa makipa mazoezini kwa namna wanavyotimiza majukumu yao anaamini kuwa wote wakiwa imara ni mwendelezo wa kuchagua nani ataanza kwenye kikosi cha kwanza,” ilieleza taarifa hiyo.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kila mchezaji ndani ya Yanga yupo tayari kwa majukumu yake.

“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kutimiza majukumu hivyo tuna amini kwamba tutafanya vizuri kwenye mashindano tunayoshiriki,”.

Previous articleVIDEO:TAZAMA MASHABIKI WA SIMBA UWANJA WA MKAPA
Next articleAMANI ITAWALE KWENYE KILA ENEO SIMBA DAY