Home Sports LUIS AMEANZA KAZI UTURUKI

LUIS AMEANZA KAZI UTURUKI

LUIS Miquissone kiungo wa Simba baada ya kujiunga na wachezaji wenzake nchini Utuki ameanza mazoezi tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Kiungo huyo wa Simba alisepa hapo 2021 na kuibukia Al Ahly ambapo huko hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba.

Hivi karibuni alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mabosi wake wa Al Ahly ambapo tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa anaweza kuibukia Azam FC ama Yanga.

Yanga walikuwa wanatajwa kutokana na kutambua uwezo wa kiungo huyo alipokuwa ndani ya Simba pamoja na Azam FC nao walimuona alipokuwa akivuja jasho.

Mwisho dili la Yanga na Azam halikujibu kama tetesi zilivyokuwa zinaeleza na badala yake amerejea kwa mara nyingine dani ya Simba.

Kiungo huyo amesema; “Nimerejea ndani ya Simba kwa mara nyingine kufanya kazi kwa mara nyingine tena nina amini tutafikia mafanikio na malengo yetu kwa kuwa kila kitu kinawezekana,” .

Anaungana na viungo wengine ikiwa ni mshikaji wake Clatous Chama, Peter Banda ambaye anavaa jezi namba 11 aliyokuwa anaivaa zama zile alipokuwa ndani ya Simba.

Previous articleROBERTINHO:MLETENI YEYOTE, MILIONI 400 ZAMSHUSHA MRITHI WA MAYELE
Next articleHAPA UJANJA WA AZIZ KI UMEJIFICHA