Home Sports UZI MPYA WA SIMBA, KIBEGI KIMEFIKA KILIMANJARO KILELENI

UZI MPYA WA SIMBA, KIBEGI KIMEFIKA KILIMANJARO KILELENI

HATIMAE ile safari ya Kibegi cha Simba imegotea kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Huu ni uzinduzi wa kwanza kwa Simba kufanya jambo hili kwa kuzindua uzi mpya kwenye mlima mrefu Afrika.

Ikumbukwe kwamba Simba ni mabalozi wa utalii wa ndani na kwenye mechi za kimataifa wana uzi wao wenye nembo ‘Visit Tanzania’.

Ni watu maalumu ambao ni mashabiki wa Simba wamefanikisha zoezi hili ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Uzi huo unapatikana kwenye maduka yote Tanzania na popote anayehitaji uzi mpya anapelekewa.

Previous articleMUVI YA WANANCHI KUPORWA MCHEZAJI NA WATANI IPO HIVI
Next articleYANGA HII IMEENDAA, CHAMA ATOA TAMKO ZITO