Home Sports SINGINDA FOUNTAIN GATE WAZINDUA UZI MPYA

SINGINDA FOUNTAIN GATE WAZINDUA UZI MPYA

KLABU ya Singida Fountain Gate imezidua uzi mpya kwa ajili ya msimu wa 2023/24 unaotarajiwa kuanza Agosti 15.

Timu hiyo uzi wake mpya una nembo ya Singida Big Stars jina ambalo lilikuwa linatumiwa na timu hiyo msimu wa 2022/23 kabla ya kubadilishwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni uchapaji wa jezi kuanza mapema.

” Jezi mpya za Singida Fountain Gate zimeingia sokoni leo Julai 19,2023 zikiwa na logo ya jina la zamani la Singida Big Stars jambo ambalo limezua maswali kwa mashabiki wetu na wadau.

“Wakati wa mchakato wa mauzo ya klabu yetu ya Singida Big Stars kwenda Singida Fountain Gate tayari mdhamini wetu wa jezi Vunja Bei Sports alikuwa ameshatengeneza jezi za msimu hivyo mchakato wa mabadiliko ukachelewa kufanyika.

“Kuepuka kuchelewa kwa jezi kama msimu uliopita na kupata hasara ya kurudisha jezi kiwandani ikapelekea hilo kutokea lakini mchakato wa kufanya mabadiliko ya logo yetu unaendelea,”.

Previous articleKIUNGO SIMBA MIKONONI KWA WAPELEKA MAUMIVU YANGA
Next articleISHU YA CHAMA, FEI TOTO NI MVURUGANO TUPU