Home Sports AZAM FC NDANI TUNISIA

AZAM FC NDANI TUNISIA

KIKOSI cha Azam FC kimewasili jijini Sousse, Tunisia kwa kambi ya wiki tatu ya maandalizi ya msimu mpya 2023/24.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Feisal Salum, Ayoub Lyanda, Idris Mbombo.

Timu hiyo ilipitia Dubai kabla ya kuibukia Tunisia kwa maandalizi ya msimu mpya.

Mchezo wa kwanza kwa Azam FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya Yanga.

Ni hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii na mshindi atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali kati ya Simba na Singida Fountain Gate.

Kwenye hitimisho la kumpata mshindi wa kwanza na watatu itakuwa ni Agosti 13,2023 palepale Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Fei Toto ni ingizo jipya ndani ya Azam FC akiwa ni mzawa wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi hicho akitokea Yanga.

Previous articleUMAKINI HAUKWEPI MUDA WA MAVUNO
Next articleMWAMBA KASEKE BADO YUPO NDANI YA SINGIDA FOUNTAIN GATE