Home Sports SportPesa YAIPA YANGA 405 MILIONI

SportPesa YAIPA YANGA 405 MILIONI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya SportPesa Tarimba Abbas amesema kuwa wanajivunia kuidhamini Klabu ya Yanga kwa kuwa imeitendea haki nembo yao na kufaya vizuri kwa msimu wa 2022/23.

Yanga imetwaa mataji matatu Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC, Azam Sports Federation kwa ushindi dhidi ya Azam FC.

Julai 10 2023 Yanga imekabidhiwa zawadi hiyo kwa kupokea hundi ya mfano wa miliono 405 kutokana na kufanya vizuri kwenye msimu wa 2022/23 kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa katika Hotel ya Serena.

Tarimba amesema: “Tunajivunia kuendelea kuwa Wadhamini Wakuu wa Klabu hii kubwa yenye mafanikio na uongozi imara. Mafanikio wanayoyapata Yanga yanakuja kutokana na kufanya kazi kwa uweledi na kuendesha klabu hii kisasa.

“Uzuri ni kwamba wanatendea haki nembo ya kampuni ya SportPesa na tunaamini kwamba wataendelea kufanya vizuri kwenye misimu ijayo,” .

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa wanatambua namna wadhamini wao wanavyofuata yale yalipo kwenye vipengele vya kimkataba.

“Napenda kuwapongeza na kuwashukuru kwa kuwa sehemu kubwa ya mafanikio haya, mmekuwa nasi kwa msimu mzima na Yanga imekuwa ikinufaika kwa kupata fedha zote zilizokuwa kwenye mkataba na sasa tunapata fedha nyingine kupitia mafanikio tuliyopata pamoja kwa msimu huu wa uliomalizika,” .

Previous articleMASHINE MBILI ZA KAZI HIZI HAPA SIMBA
Next articleVYUMA VITATU VIMEBAKI, WANNE WAFUNGA USAJILI YANGA