MANCHESTER United inapiga hesabu kuinasa saini ya Andre Onana ambaye ni kipa.
Onana anakipiga ndani ya Inter Milan akiwa ni miongoni mwa makipa bora Ulaya.
Ofa ya pauni 34.4 m zimewekwa mezani na Manchester United Kwa inter Milan pamoja na bonasi ambapo jumla inatajwa kufika pauni 38.5 m.
Inter Milan wanataka pauni 44 m kumuachia kipa huyo huku United wakiwa na uhitaji wa kipa kwani David de Gea yupo huru mkataba wake uligota mwisho Juni 30, 2023.