YANGA KUANZA KUSHUSHA VYUMA VYA KAZI

ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa tayai timu hiyo imeshakamilisha zoezi la usajili kwa ajili ya kusuka kikosi hicho.

Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2022/23 baada ya kugotea nafasi ya kwanza na pointi 78 kibindoni.

Timu hiyo ya Yanga imewapoteza wapinzani wao ikiwa ni pamoja na Simba iliyogotea nafasi ya pili huku Azam FC nafasi ya tatu na Singida Big Stars ikigotea nafasi ya nne.

Ipo wazi kwamba Julai Mosi 2023 dirisha la usajili lilifunguliwa na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

Kamwe ameema:” Tayari klabu imeshafanya usajili wa wachezaji wapya na wiki hii tutaanza zoezi la kuwatambulisha wachezaji hao kuelekea kuanza kwa msimu mpya Ligi Kuu ya NBC ambao ni msimu wa 2023/24.

“Wachezaji ambao wanakuja ni bora na imara kwa ajili ya kuleta ushindani tunaamini kwamba kila mmoja atafanya vizuri ni suala la kusubiri na kuona namna gani,” .

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni Nickson Kibabage nyota wa Singida Fountain Gate, Hassan Nassoro, Kelvin Nashon kwa upande wa wazawa.