UWEKEZAJI LIGI YA VIJANA UNAHITAJIKA

    TUMEONA namna ligi ya vijana ambavyo imekuwa na ushindani mkubwa huku baadhi ya timu zikikwama kufika hata nusu fainali.

    Hili ni somo kubwa hasa kwenye uwekezaji wa soka letu la ndani kule ambako tunahitaji kuelekea kwa kuwa ni muhimu kuwa na nguvu kwenye soka la vijana.

    Ikiwa ligi ya vijana haitakuwa na uwekezaji mkubwa inamaanisha kwamba hakutakuwa na maendeleo wakati ujao kwenye soka letu.

    Hapa unaona wakongwe Yanga na Simba bado nguvu haijawa kubwa kwenye eneo la soka la vijana jambo ambalo linaongeza gharama kwenye usajili.

    Yanga, Singida Fountain Gate, Geita Gold mpaka Namungo timu zote ni muhimu kuwekeza nguvu huku.

    Kizazi cha vijana kutoka kwenye timu hizi kubwa hakipo tena kwenye soka zaidi ya kubakiwa na simulizi za kizazi kilichopita.

    Hakika ni muhimu kuongeza nguvu kwenye eneo hili kwa ajili ya kuwa imara kwa wakati ujao kwenye lligi ya Tanzania na itaongeza uimara wa wachezaji wale watakaokuwa kwenye timu za wakubwa.

    Wachezaji wakianza kujengwa wakiwa vijana taratibu wanakuwa kwenye mfumo bora utakaokuwa unatoa matokeo mazuri kwa timu husika pamoja na taifa.

    Kama ilivyo kwa Mtibwa Sugar na Azam FC hizi ni mfano bora kwenye kukuza na kuendeleza vipaji kwa upande wa vijana na zimekuwa zikipata matokeo chanya.

    Ni muda wa kujifunza kutoka kwa timu hizi ambazo zimekuwa zikipata faida ya kuwatumia wachezaji wazawa kutoka kwenye timu za vijana.

    Bado kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha mazingira ya vijana ili wapate nafasi kucheza kwenye timu za wakubwa na baadaye kuwa katika timu ya taifa.

    Furaha ya mashabiki ni kuona mafanikio kwenye kila idara na timu kupata matokeo mazuri yote yanawezekana.

    Previous articleSIMBA KAZI IMEANZA, KAMBI ULAYA
    Next articleALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA HUYO KAIZER