MASTAA wa Simba tayari wameripoti kambini ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 unaotarajiwa kuanza Agosti.
Msimu wa 2022/23 Simba imegotea nafasi ya pili kwenye ligi huku vinara wakiwa ni Yanga.
Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi wakiwaacha kwa tofauti ya pointi tano watanitano watani zao wa jadi.
Ni pointi 78 walikomba Yanga huku Simba ikikomba pointi 73 zote baada ya kucheza mechi 30.
Baada ya kuwasili nyota hao walifanyiwa vipimo vya afya kabla ya safari ya nje ya nchi ambapo wanatarajiwa kuweka kambi.
Ni Uturuki timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira inatarajiwa kuweka kambi.
Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye vipimo ni pamoja na Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, John Bocco na Ally Salim.
Wengine wanatarajiwa kufanyiwa vipimo leo Juni 4 2023 kabla ya kukwea pipa kuelekea Ulaya kwa ajili ya kambi.