AMEANDIKA Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba kuhusu Jonas Mkude ambaye hatakuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24 namna hii:-
Ameondoka mtu tunaempenda kweli, ameondoka mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu.
Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda.
Wakati Simba ina njaa, Azam ilimhitaji hakuenda, akachagua kuvumilia njaa yetu huyu ni zaidi ya mchezaji kwetu
Sisi tulitamani Jonas Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine.
Kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu.
Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote.
Sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hiyo hiyo.