Home Uncategorized KOCHA MBRAZIL KURAHISISHIWA KAZI NDANI YA SIMBA

KOCHA MBRAZIL KURAHISISHIWA KAZI NDANI YA SIMBA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi kwenye upande wa usajili ili kuongeza wachezaji imara ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao.

Ni Roberto Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amewaomba viongozi wa timu hiyo kuongeza wachezaji wawiliwawili kila idara ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi kwa msimu ujao wa 2023/24 baada ya kushuhudia ubingwa ukienda Yanga.

Kukamilika kwa usajili ndani ya Simba kutamrahisishia Oliveira raia wa Brazil kwenye utendaji wake katika kupambania malengo ya Simba.

Simba imepishana na mataji yote iliyokuwa inapambania ikiwa ni pamoja na ligi, Azam Sports Federation, Ngao ya Jamii, Kombe la Mapinduzi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ikigotea nafasi ya pili kwenye ligi na pointi 73.

Nafasi ya kwanza ni Yanga yenye pointi 78 huku tatu ikiwa kwa Azam FC na namba nne ni Singida Big Stars.

Salim Abdallah, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba amesema wanakwenda kufanya usajili makini na utakaozingatia vigezo vyote ili kuwapa nafasi wachezaji watakaokuja kuonyesha uwezo wao.

“Kwa namna ambavyo tumefanya kwenye ligi hatujapenda kwani malengo yetu hayajafikiwa hivyo ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa yaliyopita na kufanya usajili mzuri kwenye kila idara.

“Kikubwa ambacho tunahitaji kwa msimu ujao ni kuwa tofauti na kupata kile ambacho tunahitaji. Usajili wetu ujao tunaamini utakuwa mzuri na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa kwani tunaendelea vizuri,”.

Previous articleYANGA:HATUNA JAMBO DOGO
Next articleVIDEO:SABABU YA YANGA KUMPA KAZI KOCHA IBENGE