MUDA WA KAZI KWA AJILI YA MSIMU UJAO NI SASA

    NYAKATI zinakuja na kupita na sasa ni wakati wa maandalizi ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote baada ya mabingwa wa ligi ambao ni Yanga kutangazwa.

    Ipo wazi kuwa kesi ya ubingwa kwenye kila eneo kuanzia Ligi Kuu Bara, Azam sports Fedaration mpaka suala la tuzo zote zimefungwa.

    Tumeona namna Singida Big Stars ambavyo wameleta ushindani kwenye ligi Namungo mpaka Geita Gold namna hali ilivyokuwa kazi.

    Kila mmoja ameona kile ambacho amekivuna na kupanda wakati wa mwanzo wa msimu namma ambavyo kimeleta matokeo mazuri.

    Kwa waliofanikiwa kwa asilimia kubwa pongezi wanastahili na kwa wale ambao wamekwama kwa asilimia kubwa ni muhimu kuangalia wapi ambapo walikosea.

    Kikubwa ni kuona wakati ujao kila kitu kinakuwa kwenye mpangilio mzuri na wachezaji wanatimiza majukumu yao kwa umakini.

    Tunaona kuna masuala ya kuwa kwenye mashindano ya kimataifa katika hili ni lazima kila mchezaji kutimiza majukumu yake kwa umakini.

    Kila mchezaji anatambua kile ambacho alikifanya kwa msimu huu ambao umgota mwisho na kila mmoja kupata alichokivuna na sasa ni muda wa maandalizi ya wakati ujao.

    Kazi bado haijaisha kwa kuwa msimu mpya unakuja na kila mchezaji anatambua kwamba akipata changamoto mpya ni lazima apambane kutimiza majukumu yake.

    Ukweli ni kwamba kila mmoja anapenda kufanya vizuri akipata kazi kwenye timu mpya hivyo kwa makosa ambayo yametokea msimu huu ni muhimu kila mmoja kufanyia kazi.

    Muda wa kufanyia kazi yote hayo ni sasa ukizingatia kwama ni nyakati za kusaka ushindi kwa kuwa hakuna kiongozi anayependa kuona timu inashindwa kupata matokeo hata wachezaji pia.

    Mashabiki nao furaha yao ipo kwenye ushindi na wamekuwa wakijitoa kwenye mechi zilizochezwa kwa kila mmoja kuipambania timu kwa kushangilia bila kuchoka.

    Muda ambao upo kwa sasa ni kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na tunaamini kwamba kila mmoja atafanyia kazi yale makosa ambayo kajifunza kwenye msimu huu.

    Tunaamini kwamba malengo ya timu na kufanya kazi yale ambayo yalikuwa yanafanya masuala yasiende vizuri muda ni sasa na kila kitu kinawezekana.

    Kila atakayepewa majukumu wakati ujao itapendeza akifanya kwa umakini sio mchezaji pekee bali mpaka mashabiki ni muhimu kuendelea kujitoa kwa ajili ya kushangilia timu zao.

    Ushindani unahitaji washindani wale wa kweli na wachezaji ambao wataanza maandalizi vibaya kuna uwezekano wakashindwa kuwa kwenye mwendo bora.

    Hakuna ambaye anapenda kuona wachezaji wakikwama kuwa kwenye mwendo mzuri ni muhimu kwa sasa kuanza maandalizi mazuri.

    Ukweli ni kwamba ligi imekuwa na ushindani mkubwa na kila mchezaji ameona pamoja na benchi la ufundi limeshuhudia hivyo wakati ujao nao utakuwa bora zaidi.

    Kwa sasa ni muda mfupi unaonekana hasa ukizingatia kwamba wale ambao wanapambana kufikia malengo yao ni lazima wajitoe kwa juhudi pamoja na maarifa.

    Wakati ni sasa kupanga mipango mipya na nyakati bora hazidumu muda wote kama ilivyo nyakati ngumu ni lazima zifike mwisho.

    Previous articleVIDEO: KISUGU AMFUNGUKIA MAYELE WA YANGA
    Next articleVIDEO:JEMBE AWAVAA VIONGOZI YANGA/MAYELE,DIARRA,BANGALA KUONDOKA