Home Sports SIMBA KUSHUSHA MITAMBO YA KAZI

SIMBA KUSHUSHA MITAMBO YA KAZI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utaingia sokoni kuleta mtambo wa mabao utakaoongeza kasi kwenye idara hiyo kwa msimu wa 2023/24.

Timu hiyo imegotea nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara ni Yanga ambao wametwaa ubingwa wa ligi.

Ikumbukwe kwamba Yanga walikuwa wanatetea taji hilo walilotwaa msimu uliopita 2021/22.

Ipo wazi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira aliomba kuongezewa kiungo mshambuliaji mwenye kasi kama Saido Ntbanzokiza ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Oliveira amesema kuwa anahitaji kuwa na kiungo kama Ntibanzokiza ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo mshambuliaji pale Ntibanzokiza anapokuwa hayupo fiti.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema kuwa hawatafanya makosa kwenye usajili kwa kuwa wanajua aina ya wachezaji wanaotakiwa.

“Wale wachezaji ambao wanatakiwa na benchi la ufundi hao watakuja na nimeona namna ambavyo tunafanya kazi kwa umakini tutaleta wachezaji wenye ubora ambao watakuwa na nafasi yakuleta ushindani kwenye kikosi.

“Kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka wakati unakuja na tutafanya kazi kwa umakini kwani msimu huu tunajua hatujafanya vizuri hivyo tunajipanga kwa wakati ujao,” amesema Ally.

Previous articleBILIONI 2.8 ZAMPELEKA MAYELE UARABUNI
Next articleBEKI WA KAZI YANGA KUKUNJA MKWANJA MREFU