Home Sports KOCHA ALIYEPELEKA MAUMIVU MSIMBAZI SAFARI IMEMKUTA

KOCHA ALIYEPELEKA MAUMIVU MSIMBAZI SAFARI IMEMKUTA

KALI Ongala aliyekuwa kocha msaidizi wa Azam FC hatakuwa kàtika benchi hilo kwa msimu wa 2023/24.

Kocha huyo amepeleka maumivu kwa Simba mara mbili kwenye mashindano tofauti ligi na shirikisho.

Ongala mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa Juni 12 aliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Azam FC 0-1 Yanga.

NI fainali ya Azam Sports Federation licha ya timu hiyo kutengeneza nafasi nyingi kupitia Kwa Prince Dube na Sopu ngoma ilikuwa ngumu kwake kushinda mbele ya Yanga chini ya Nasreddine Nabi.

Bao pekee la ushindi Kwa Yanga lilipachikwa na Kennedy Musonda dakika ya 14 likadumu mpaka mwisho na kombe likawa Mali ya Yanga.

Ni mechi 32 ameongoza akishinda 21, Sare nne na kupoteza mechi 7 katika mashindano yote.

Kwenye mechi ambazo ameshinda katika Ligi Kuu Bara ni moja dhidi ya Simba kwa bao moja la Dube Uwanja wa Mkapa na nyingine kwenye Azam Sports Federation ilikuwa mabao 2-1 dhidi ya Simba Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Previous articleKOCHA YANGA KUIBUKIA SIMBA
Next articleYANGA SC:KOCHA ANAYEKUJA ATATIKISA NCHI, FAGIO LAPITA SIMBA