Home Uncategorized WAKALI WA KUTENGENEZA PASI ZA MWISHO BONGO

WAKALI WA KUTENGENEZA PASI ZA MWISHO BONGO

WAKALI ni wakali tu iwe ni mwanzo ama mwisho wanakiwasha na msimu wa 2022/23 umeshuhudia wengi kwenye kila sekta.

Kwenye mwendo wa data tuna wakali wa kutengeneza pasi za mwisho namna hii:-

Clatous Chama pasi 14

Kinara kwa kutengeneza pasi za mwisho Bongo ndani ya Ligi Kuu Bara ni Clatous Chama yupo zake ndani ya Simba ambapo alitoa jumla ya pasi 14 huku akitupia mabao mawili kibindoni.

Rekodi zinaonyesha kuwa Chama alitoa pasi 7 kipindi cha kwanza na 7 kipindi cha pili na mabao yake manne, alifunga mawili kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili yeye ni raia wa Zambia.

Saido Ntibanzoiza pasi 12

Ntibanzokiza aliibuka ndani ya Simba akitokea Geita Gold ambapo akiwa huko alitoa jumla ya pasi sita za mabao.

Majukumu yake ndani ya Simba mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Tanzania Prisons alipotoa pasi yake ya kwanza ilikuwa Desemba 30,2022 Uwanja wa Mkapa.

Anafunga msimu akiwa ametoa pasi sita za mabao pia ndani ya Simba zinazofanya afikishe jumla ya pasi 12 za mabao kibindoni.

Ayoub Lyanga pasi 8

Ndani ya Azam FC mwamba Ayoub Lyanga anaingia kwenye orodha ya mastaa wenye pasi nyingi ndani ya ligi akiwa nazo 8 kibindoni.

Mzawa huyu ni chaguo la kwanza la Kali Ongala akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga mapigo huru ambapo alimpa mshikaji wake Daniel Amoah pasi mbili kutokana na mapigo huru moja ilikuwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa na nyingine ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Shomari Kapombe pasi 8

Muweke kati anakiwasha hata pembeni yupo ni Kapombe beki mwenye pasi nyingi kuliko wote ndani ya ligi msimu wa 2022/23 akiwa ni mali ya Simba.

Pasi yake ya nane alimpa Ntibanzokiza mchezo dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Uhuru na pasi yake ya 7 ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania alimpa mshikaji wake huyohuyo na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Sixtus Sabilo pasi 7

Winga mzawa ambaye alikuwa na kasi kubwa mwanzo mwa msimu ila upepo ulipobadilika hakuwa kwenye makali aliyoanza nayo akigotea kwenye kutoa pasi 7 za mabao na kufunga mabao 9 yupo ndani ya Mbeya City.

Nicolas Gyan pasi 6

Beki wa Singida Big Stars uwezo wake kumwaga majalo upo akiwa na mshikaji wake Meddie Kagere wanaiva chungu kimoja akiwa na pasi zake sita.

Mohamed Hussein pasi 6

Nahodha msaidizi wa Simba kwenye mechi za kufungia msimu mbili hakuwa kwenye eneo la uwanja lakini jumla ana pasi sita za mabao.

Aziz KI pasi 5

Mtaalamu wa kutumia mguu wa kushoto, pasi zake zote za mabao ametoa kwa mguu huo n ahata mabao yake 9 pia kafunga kwa mguu wa kushoto kiungo huyu wa Yanga.

Jesus Moloko pasi 5

Mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu ndani ya Yanga ni Moloko kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ni pasi tano anazo kibindoni.

ReplyForward

Previous articleCITY MABINGWA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Next articleNTIBANZOKIZA NA TUZO MKONONI, MABAO SABABU