UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utarejea kwenye mashindano ya kimataifa wakati mwingine ukiwa imara zaidi.
Timu hiyo kutoka Tanzania imeandika rekodi nzuri ya kucheza fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni ya kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.
Imegotea kuwa mshindi wa pili baada ya ushindi wa jumla ya Yanga 2-2 USM Alger kuwabeba Waarabu wa Algeria ambao walishuhudia Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 1-2 USM Alger.
Ugenini ubao ulisoma USM Alger 0-1 Yanga hivyo kila timu imeshinda ugenini lakini kwa wapinzani wa Yanga wamefaidika na ushindi wa ugenini.
Miongoni mwa wachezaji ambao wamvaa medali ndani ya Yanga ni pamoja na mzee wa kuchetua Bernard Morrison, Fiston Mayele mkali wa kucheka na nyavu, Dickson Job na Farid Mussa.
Kikosi hicho tayari kimewasili Dar na leo Juni 5 kimepewa mualiko Ikulu kwa ajili ya pongezi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.