YANGA WAPEWA HEKO NA RAIS SAMIA, WAITWA IKULU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameialika timu ya Yanga kwenye hafla ya chakula cha jioni Juni 5, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Juni 4 imeeleza hivyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais ameialika Yanga kwenye hafla ya chakula cha jioni Juni 5,2023 Ikulu Jiji Dar kwa lengo la kuipongeza kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF) yaliyohitimishwa jana Juni 3, 2023 Jijini Algers nchini Algeria.

Yanga ni mshindi wa pili baada ya ushindi wa jumla ya mabao 2-2 kwa timu zote mbili ambapo kila mmoja alishinda mechi za ugenini.

USM Alger walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 1-2 USM Alger na ule uliochezwa Uwanja Juni 5 ukisoma USM Alger 0-1 Yanga na bao mtupiaji akiwa ni Djuma Shaban.

Yanga imekamilisha fainali ya pili ikiwa imeshinda lakini haijatwaa taji kutokana na faida la bao la ugenini lililowapa faida USM Alger.