AZAM FC KUFUNGA MSIMU NA KETE HIZI

UONGOZI wa Azam FC umebainisha kuwa unatarajia kufunga msimu wa 2022/23 kwa mechi tatu za jasho na damu.

Kwenye mechi hizo moja itakuwa ni fainali dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Tanga.

Timu hiyo kwa sasa inaendelea na maandalizi kwa mechi hizo zilizobaki ili kupata matokeo mazuri.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema wanatambua kazi iliyopo mbele yao ni mechi ngumu ila watapambana kufanya vizuri.

Ibwe amesema:”Timu kubwa inabidi ifanye kazi kubwa na tunafunga msimu wetu mwezi Juni kwa kucheza mechi tatu za jasho na damu ambazo zitakuwa na ushindani mkubwa.

“Kwenye hizo ni mechi mbili tutakuwa tukimalizia Ligi Kuu ya NBC, kwa kucheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Polisi Tanzania.

“Mchezo wetu wa mwisho ambao tutafunga msimu itakuwa kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), dhidi ya Yanga, Juni 12 Uwanja wa Mkwakwani,”.