Home Sports USM ALGER MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

USM ALGER MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

USM Alger ya Algeria inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Yanga.

Ushindi wa jumla ya mabao 2-2 haujawapa fursa Yanga wawakilishi kutoka Tanzania kutwaa taji hilo.

Katika mchezo wa leo Yanga imeshuhudia ubao wa Uwanja wa Juali 5 ukisoma USM Alger 0-1 Yanga huku mtupiaji akiwa ni Djuma Shaban dakika ya 6 kwa mkwaju wa penalti..

Pongezi kwa Djigui Diarra ambaye alitimiza majukumu yake kwa umakini kwa kuokoa hatari ikiwa ni pamoja na penalti katika mchezo wa leo Juni 3.

Katika mchezo wa fainali ya kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-2 USM Alger hivyo bao la ugenini limewapa taji wapinzani wa Yanga.

Previous articleMASTAA SIMBA KWENYE MAJUKUMU MENGINE
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE SPOTI XTRA JUMAPILI