Home Sports WANANCHI KIMATAIFA UGENINI WANA ZALI

WANANCHI KIMATAIFA UGENINI WANA ZALI

WAKATI leo Juni 3 Yanga ikitarajiwa kutupa kete ya pili kwenye mchezo wa fainali dhidi ya USM Alger ya Algeria rekodi zinaonyesha kuwa wamekuwa wakifanya balaa ugenini.

Katika mechi 11 ambazo Yanga wamecheza baada ya kutinga hatua ya makundi ni mechi tano ilicheza ugenini huku ikiambulia kichapo kwenye mechi moja pekee.

Rekodi zinaonyesha kuwa Yanga imepata ushindi kwenye mechi tatu na kuambulia sare ya kugawana pointi mojamoja kwenye mchezo mmoja ugenini.

Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Fiston Mayele mwenye jumla ya mabao saba ugenini imefunga mabao sita huku ukuta unaoongozwa na Bakari Mwamnyeto mwenye pasi mbili za mabao kwenye anga la kimataifa umetunguliwa mabao matatu.

Mechi hizo ilikuwa namna hii:-US Monastri 2-0 Yanga mchezo huu ulichezwa Februari 12,2023, Real Bamako 1-1 Yanga ilikuwa Februari 26, kigongo kingine ilikuwa TP Mazembe 0-1 Yanga Aprili 2.

Walipokabiliana na Rivers United 0-2 Yanga ngoma ilipigwa Aprili 23 katika hatua ya nusu fainali ya pili ugenini ilikuwa Marumo Gallants 1-2 Yanga ngoma ilipigwa Mei 13, Afrika Kusini.

Previous articleYANGA KAMILI KUWAVAA WAARABU KIMATAIFA
Next articleZIMEMALIZA TOP 4 ULAYA MARA NYINGI ZAIDI