Skip to content
UBAO wa Uwanja wa Julai 5 nchini Algeria unasoma USM Alger 0-1 Yanga ikiwa ni dakika 45 za kwanza.
Mchezo kwa sasa ni mapumziko ambapo Yanga imepata bao la mapema katika fainali ya pili itakayoamua mshindi wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Bao la kuongoza kwa Yanga limefungwa na Djuma Shaban dakika ya 6 kwa pigo la penalti.
Kipa Djigui Diarra amekuwa kwenye umakini katika kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja akiokoa hatari za wapinzani.