Home Uncategorized KUSHINDWA LEO MWANZO WA KUPAMBANA KESHO

KUSHINDWA LEO MWANZO WA KUPAMBANA KESHO

MAISHA ya mpira yanahitaji umakini mkubwa kwa kila mmoja kupambana kutimiza malengo ambayo yapo kwenye timu husika na inawezekana licha ya kwamba msimu unakaribia kufika ukingoni.

Tumeona kwamba kila timu imefanya kazi yake kwa kupambana kufikia malengo na wapo ambao walikwama na wengine wanasubiri mpaka mechi mbili za mwisho kukamilisha hesabu huku Yanga wakiwa wametwaa ubingwa.

Haifiki mwisho mpaka itakapokuwa mwisho hivyo muhimu kujipanga kwenye kila idara katika kupambana kusaka ushindi ndani ya uwanja hata kwa Singida Big Stars.

Dakika 90 zina maana kubwa kufanya yale maagizo kutoka kwenye benchi la ufundi kwa kuwa wanatambua ili kupata ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki ni lazima kuwepo na kikosi kazi kweli.

Kwa kukwama kufikia malengo msimu ambao unakaribia kuisha haina maana ni lazima kukata tamaa hilo lisipewe kipaumbele kwa kila mmoja.

Mpira ni uwekezaji na pale ambapo timu imefeli kwenye kuwekeza ina muda wa kuangalia upya makosa na kufanya kweli kwa ajili ya wakati ujao.

Kwenye anga la kimataifa tumeona zile timu ambazo zilianza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na nyingine kugotea kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kila mmoja alikuwa anapambania jambo lake.

Kushindwa kufanya vizuri leo haina maana kwamba na kesho itakuwa hivyo hapana ni muhimu kuwa na mwendelezo mzuri wa kufanyia maboresho makosa.

Kushindwa kupata matokeo uwanjani leo ni mwanzo wa kujipanga kwa ajili ya kesho.

Previous articleMKATA UMEME SIMBA KUCHOTA MILIONI 350
Next articleVIDEO:YANGA:MAYELE ATAWAFUNGA WAARABU TENA