Home Uncategorized CHAMA AWAPA TUZO MASTAA SIMBA

CHAMA AWAPA TUZO MASTAA SIMBA

CLATOUS Chama kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba ameweka wazi kuwa ikiwa atakosa tuzo ya kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara kisha wakachukua nyota wengine anaocheza nao ndani ya Simba kwake itakuwa furaha.

Simba imegotea nafasi ya pili na vinara ni watani zao wa jadi Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yanga pia ni mabingwa wa msimu wa 2022/23 baada ya kufikisha pointi 74.

 

Jina la Chama ni miongoni mwa mastaa wanaowania tuzo ya kiungo bora ndani ya ligi msimu wa 2022/23 akiwa pamoja na Mzamiru Yassin na Saidi Ntibanzokiza wote wanakipiga ndani ya Simba.

Kiungo huyo ni namba moja kwa nyota wenye pasi nyingi za mabao akiwa nazo 14 kibindoni. Ametupia mabao manne.

Kahusika katika mabao 18 kati ya mabao 66 yaliyofungwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 67.

Nyota huyo amesema:” Kuwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ni jambo zuri lakini muhimu kuona wachezaji wenzangu hili wanalipokeaje.

“Ukweli ni kwamba hatujawa na msimu mzuri uwanjani kutokana na matokeo ambayo tumeyapata hivyo Kwa yalitotokea tunafanyia kazi.

“Nimeona kuna majina matatu kutoka Simba ikiwa ni mimi, Mzamiru Yassin na Saidi Ntibanzokiza umakini mkubwa katika yao. Nina amini wakichukua itakuwa  furaha kubwa pia,”

Previous articleWASIWASI DAWA, WAARABU SIO WA KUWABEZA
Next articleUSM ALGER:HATUCHEZI NA MAYELE SISI