MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp ameweka wazi kuwa licha ya timu hiyo kukwama kumaliza ndani ya nne bora bado wachezaji walikuwa na ushirikiano mkubwa.
Amebainisha kuwa licha ya kukatishwa tamaa kwa kukosa kufuzu kwa soka ya Ligi ya Mabingwa, Klopp amesifu umoja wa wachezaji na wafuasi baada ya kuwa kwenye msimu mgumu.
Mshambuliaji Mohamed Salah alitweet kuwa “alihuzunishwa” baada ya kushindwa kumaliza katika nafasi ya nne bora. Lakini Klopp anasema kuna sababu za kuwa na matumaini timu hiyo itamaliza msimu kwa mchezo dhidi Southampton Jumapili, saa 4.30 usiku
Ni msimu wa kwanza katika kipindi kirefu cha Klopp ambapo Liverpool haijajikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo na baada ya ushindi wa Manchester United dhidi ya Chelsea kuthibitisha hilo Alhamisi jioni, mfungaji bora wa timu hiyo Mohamed Salah alitweet kuwa “amehuzunishwa”.
Klopp alikubali kuwa lilikuwa pigo chungu na alikubali kuwa kulikuwa na ‘makosa’ yaliyofanywa msimu wote lakini akasisitiza kuwa kuna sababu nyingi za mashabiki wa Liverpool kuwa na matumaini juu ya kile kinachotokea mbele.
“Kwangu ilikuwa wazi timu zingine mbili [Newcastle na Man Utd] zingepata alama hiyo [zilihitaji kupata kandanda ya Ligi ya Mabingwa],” alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa mwisho wa Liverpool wa msimu huu dhidi ya Southampton Jumapili.