Home Sports SERIKALI YAENDELEZA NEEMA KWA YANGA KIMATAIFA

SERIKALI YAENDELEZA NEEMA KWA YANGA KIMATAIFA

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameunga mkono hamasa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua tiketi 1,000 za mchezo wa fainali kati ya Yanga dhidi ya USM Alger.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili ambapo hamasa zimeendelea kwa sasa mpaka Mei 28 siku ya mchezo.

Rais Samia amekuwa na timu zote bega kwa bega kwenye sekta ya michezo ambapo kwenye anga la kimataifa amekuwa akitoa hamasa kwa kununua kila bao ambalo linafungwa.

Simba kabla haijaondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika nayo ilikutana na zali la bao la mama huku mechi iliyowapa mkwanja mrefu ilikuwa ile waliyoshinda mabao 7-0 Horoya.

Kwa sasa katika hatua ya fainali bao la mama thamani yake ni milioni 20 na ameahidi kuwa hata yakifungwa mabao mangapi hakuna tatizo fedha ipo kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Huu ni mwendelezo wa neema kwa Yanga kwa kuwa Rais Samia Mei 22 alitoa zawadi ya tiketi 5,000 kwa mashabiki wa Yanga ili wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa.

Previous articleINJINIA AFUNGUKIA ISHU YA MKATABA WA FEISAL
Next articleYAJUE MAJEMBE YA KAZI NDANI YA SIMBA