NEWCASTEL UNITED HAO LIGI YA MABINGWA ULAYA

SASA Newcastle United uhakika kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa mara ya kwanza tangu 2003 baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Leicester.

Kikosi cha Eddie Howe kilijihakikishia nafasi ya nne bora kwa kuonyesha uwezo mkubwa na kuwaacha wageni ambao walipiga shuti moja pekee kwenye lango la wapinzani.

Newcastle walidhibiti mechi lakini walichanganyikiwa na mchanganyiko wa safu ya ulinzi ya Leicester na uchezaji wao.

Leicester walifanya juhudi moja pekee katika dakika ya 92 wakati Nick Pope alipookoa kwa kasi mpira wa Timothy Castagne na kuwanyima ushindi muhimu.