NGOMA ILIKUWA NZITO KWA WAKULIMA, JANGWANI WAKAPETA

  KILA mmoja anafuata njia zake ambazo zitampa mafanikio akikwama kidogo kupotea ni hatua inayofuata asipojipanga itakuwa kazi nyingine.

  Ilikuwa hivyo Uwanja wa Liti, njia za Singida Big Stars wakulima wa alizeti njia ziliwagomea na zile za Yanga zikawapa ushindi baada ya dakika 90.

  Ngoma fainali ya Azam Sports Federation itakuwa ni Azam FC v Yanga, Tanga, hapa tunakuletea namna njia zizivyochorwa namna hii:-

  Metacha Mnata

  Aliibuka Yanga akitokea Singida Big Stars kwenye dirisha dogo na ameanza kazi katika mchezo dhidi ya mabosi wake wa zamani alikaa langoni.

  Ni hatari dakika ya 9, 51 aliokoa alichezewa faulo dakika ya 21 na Franciy Kazad ambaye alionyeshwa kadi ya njano ya kwanza na alimchezea faulo kwa mara nyingine dakika ya 76 alisepa na dakika zote 90.

   Djuma Shaban

  Shuhuda wa timu ya Yanga ikitinga hatua ya fainali Azam Sports Federation huku ukuta wao ukiwa haujatunguliwa ugenini.

   Joyce Lomalisa

  Mwamba huyu alichezewa faulo dakika ya 45 katika mchezo huo uliokuwa na matumizi makubwa ya nguvu mwanzo mwisho.

   Bakari Mwamnyeto

  Nahodha mzawa Nondo alionyesha kazi yake akiokoa hatari dakika ya 65 alikutana na mkato wa kimyakimya dakika ya 59.

  Ukuta wao haukuruhusu kutunguliwa kwenye mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ya pili.

  Mamadou Doumbia

  Beki wa kazi aliokoa hatari dakika ya 8, 9, 12, 50, 53, 55 alikwama kusepa na dakika 90 alisepa na dakika 64 Dickson Job aliingia kukamilisha ngwe iliyobaki.

   Zawadi Mauya

  Kiungo Mauya alisepa na dakika 90 mazima akiokoa hatari dakika ya 45 na muda aliotoka Doumbia alirejea nyuma kuongeza nguvu ya ulinzi mpaka alipoingia Job kukaa kwenye eneo lake.

  Jesus Moloko

  Moloko ni miongoni mwa nyota waliokuwa na shauku ya kulisaka lango la Haule, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 59. Alikuwa anakula sahani moja na Shafiq Batambuze aliyeoonyeshwa kadi ya njano dakika ya 38.

  Alisepa na dakika 77 aliingia mzee wa spidi 120 wakumuita Tuisila Kisinda ambaye alikamlisha dakika zilizobaki.

  Salim Aboubhakari, ‘Sure Boy;

  Kiungo wa kazi alipiga kazi eneo lake akiwa na kazi ya kupiga krosi kama alivyofanya dakika ya 63 Uwanja wa Liti.

  Clement Mzize

  Kagotea kwenye mabao sita kwenye mashindano haya na bado mchezo mmoja wa fainali dhidi ya Azam FC.

  Kwenye eneo la ushambuliaji alichezewa faulo dakika ya 10 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 22 alisepa na dakika 77 aliingia Kennedy Musonda aliyekuwa akipambana na Pascal Wawa aliyeokoa hatari dakika ya 65, 66 na alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 61, 65..

  Aziz KI

  Kiungo wa kazi Aziz KI alianza kikosi cha kwanza alipiga faulo dakika ya 9, 72 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 27, 30, 53, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 53.

  Ni dakika 77 alisepa nazo akaingia Fiston Mayele  ambaye alipachika bao dakika ya 82 akiwa ndani ya 18 alipomtungua Haule bao pekee la ushindi.

   Farid Mussa

  Kiungo Farid Mussa alipiga krosi dakika ya 63 alisepa na dakika 64 ngoma ilichukuliwa na Dennis Nkane kwenye mchezo huo.

  Nyota huyo alikuwa kwenye eneo la kiungo kama Aziz Andambwile ambaye alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 64.

  Previous articleNEWCASTEL UNITED HAO LIGI YA MABINGWA ULAYA
  Next articleSAUTI:MWAMBA HUYU ATAJWA KUTUA YANGA